KITENGO CHA UHAMASISHAJI NA VIJANA

    Utangulizi

    Kitengo kilianzishwa rasmi mwaka 2016 baada ya kubaini kuwa waajiriwa wengi ni Vijana na wana jukumu kubwa la kujenga Uchumi wa Nchi. Lengo kuu la kitengo ni kuratibu na kukuza mawasiliano baina ya Wafanyakazi Vijana, kukuza maendeleo kwa Wafanyakazi Vijana na kuwawezesha kuendesha kampeni za Uhamasishaji kwenye maeneo yao ya kazi.

    Kazi za Kitengo

    1. Kutoa Elimu ya Vyama vya Wafanyakazi kwa wafanyakazi,

    2. Kutangaza Majukumu ya Chama (TUICO) katika vyombo mbalimbali vya Habari na mitandao ya kijamii,

    3. Kuratibu programu za Vijana katika Chama na

    4. Kuhamasisha na kuingiza Wanachama wapya katika Chama