TUICO NEWS

DHANA YA AFYA NA USALAMA KAZINI

Published on 2018-08-21 06:24:22
By Silpha Kapinga

UTANGULIZI
Usalama na Afya Kazini (OHS) ni azma mahususi inayolenga kulinda Usalama, Afya na Ustawi wa watu wote walio katika ajira
iliyo rasmi.

Suala la Usalama na Afya Kazini linajumuisha pia kuwakinga/ kuwalinda wafanyakazi wengine wanafamilia, waajiri, wateja, watoa huduma pamoja na jamii iliyozunguka ambao kwa njia moja au nyingine wanaweza kudhurika na mazingira ya sehemu ya kazi.

USALAMA NA KAZI
Usalama unajumuisha mazingira huru yasiyo na ajali, mikwaruzo ya mwili na kudondokewa na vitu. Usalama Kazini unaweka mazingira huru ya kutokuwa na ajali.

Mikwaruzo ya mwili au vitu vidondokeavyo watu ndio vilivyozoeleka kutambulika kuwa ni madhara ya kutokuwa na usalama kwenye maeneo ya kazi. Pia maumivu yatokanayo na michubuko au mikwaruzo ni matokeo ya mara mtu aumiapo au ni madhara yanayotarajiwa baada ya mfanyakazi kuumia.

Wafanyakazi wengi pia hupata madhara makubwa na hata kufa endapo vitu vyenye ncha kali au vitu vinavyofanana na hivyo vimwangukiapo kichwani ikiwa mfanyakazi hakuvaa vifaa vya kinga (Protective gears).

Hivyo usalama kazini inadhamiria kuweka mazingira huru ya kutopata ajali ambayo yangesababisha madhara kwa mfanyakazi. Usalama huhusisha kudhibiti nguvu zaziada katika maeneo ya kazi kwa mfano:-

? Mvuto wa nguvu za ziada
? Nguvu ya uwezo wa uzalishaji (kwa mtu)
? Nguvu ya vitu
? Nguvu za mashine
? Nguvu za magari na jumuiya (watu)
? Nguvu za umeme
? Nguvu za moto na joto
? Nguvu za kemikali n.k.
Ni dhahiri kuwa mtu huweza kukingwa / kuepushwa na madhara haya. Kama mwili wa mwanadamu utakuwa umewekwa katika mazingira hatarishi kwa kiwango kikubwa, matokeo yake ni madhara makubwa yatakayosababisha ulemavu au ajali mbaya.

Afya hujumuisha kutokuwa na maradhi yoyote mwilini. Maradhi yanaweza kusababishwa na maambukizi mbalimbali kutoka kwenye vimelea vya kibaiolojia, lakini pia yanaweza kuwa ni matokeo ya kuwa katika mazingira hatarishi ya kazi za kila siku

kwa muda mrefu. Kwa mfano:-

? Kemikali
? Kelele, joto, mionzi
? Matumizi ya mitambo na madhara ya kiigonomia

? Visababishi vilivyo katika jamii

Endapo nguvu kubwa itatumika wakati wa kutumia kemikali (mfano wakati wa kumwaga kemikali), madhara ya moja kwa moja huweza kutokea.

Hivyo kwa kawaida matumizi ya nguvu kidogo huhitajika katika tathimini ya udhibiti unaofaa kuhakikisha madhara na magonjwa yanayoweza kutokea yanapunguzwa.


Read More of this Article in TUICO Newsletter

Mtendaji wa TUICO Ndg. T. Mkolokoti akiwahamasisha Wafanyakazi kujiunga na TUICO.

............................................................................................................

Other articles

WAJIBU NA HAKI ZA VIONGOZI WA TUICO KWA MWAJIRI KATIKA UBORESHAJI WA UTENDAJI KAZI

Utangulizi ajibu na haki za Viongozi wa TUICO kwa Mwajiri katika uboreshaji wa Utendaji kazi ni pamoja na:-

published on 2018-08-21 06:59:09
By Willy Kibona

CALL FOR PROPOSALS

Call for proposals to supply TUICO with an accounting software. Deadline COB 30th May 2019 [VIEW FILE]

published on 2019-05-15 04:56:46
By Sebastian Okiki

PROHIBITING VIOLENCE AND HARASSMENT IN THE WORLD OF WORK

More than 800 million women have experienced some form of violence and harassment, ranging from physical assault to verbal abuse, bullying and intimidation...

published on 2019-06-10 04:27:32
By TUICO and IUF