TUICO NEWS

WAJIBU NA HAKI ZA VIONGOZI WA TUICO KWA MWAJIRI KATIKA UBORESHAJI WA UTENDAJI KAZI

Published on 2018-08-21 06:59:09
By Willy Kibona

Wajibu na haki za Viongozi wa TUICO kwa Mwajiri katika
uboreshaji wa Utendaji kazi ni pamoja na:-

1. Kuboresha na kuendeleza hali nzuri ya Wafanyakazi kazini

2. Kushirikiana na kujadiliana na Waajiri kuunda Mabaraza ya Wafanyakazi

3. Kudumisha amani mahali pa kazi
Kujadili, kufunga na kusimamia utekekelezaji wa Mikataba ya Hali Bora za Kazi

4. Kusimamia utekelezaji wa TUZO, Kanuni za Utumishi na Sheria nyingine za Kazi

5. Kushirikiana na kubadilishana ujuzi na Vyama vingine vya Wafanyakazi

6. Kuwasiliana na Serikali kuhusu hoja ya kutunga Sheria sahihi za kazi na kuandaa Sera nzuri za kuendeleza uchumi na maisha ya jamii

7. Kulinda maslahi ya
Wafanyakazi


Haki za Viongozi wa TUICO
kwa Mwajiri

Majukumu na Haki za Viongozi wa TUICO kwa mujibu wa kifungu cha 62(4) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.
6 ya mwaka 2004 na Katiba ya TUICO Ibara ya 7.4.1. ni pamoja na:-

A. Kuwawakilisha Wanachama kwenye malalamiko, vikao vya nidhamu na migogoro ya kikazi

B. Kushauriana na Mwajiri juu ya uzalishaji, kukuza tija na kuendeleza ajira

C. Kukiwakilisha Chama kwenye masuala ya ukaguzi na uchunguzi kwa mujibu wa Sheria za Kazi

D. Kutoa hoja kwa niaba ya Wanachama juu ya Kanuni za Afya, Usalama na Ustawi

E. Kuhamasisha na kuingiza
Wanachama wapya

F. Kusimamia Mapato na Matumizi ya fedha za Chama katika Tawi

G. Kutunza kitabu cha kumbukumbu cha Wanachama

H. Kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za Chama kwa Katibu wa Mkoa

I. Kuendeleza uhusiano bora na Mwajiri mahali pa kazi

J. Kushirikiana na Katibu Mkuu au Mwakilishi wake katika Majadiliano ya pamoja na Mwajiri

K. Kuhakikisha Wanachama wanatimiza wajibu wao kwa mujibu wa Katiba

L. Kutoa taarifa kwa Katibu wa Mkoa juu ya mgogoro wa kikazi unaoweza kusababisha kuzorota kwa kazi kwa hatua zaidi.

M. Kupokea, kuwasilisha, kutekeleza na kusimamia utekelezaji wa maagizo na maelekezo ya ngazi za juu za Chama.

Wajibu na Haki kwa Mwajiri


1. Kuendeleza uhusiano bora na matawi mengine

2. Kutekeleza makubaliano
yaliyo?kiwa na Mwajiri


Kusimamia Tija na Ufanisi

Uboreshaji na utendaji kazi unaoleta tija kiongozi wa TUICO anatakiwa kufanya yafuatayo:-

? Kuhakikisha malalamiko ya Wafanyakazi sehemu ya kazi yanatatuliwa kwa wakati

? Kuhakikisha Kanuni za Ajira zinaeleweka na kutekelezwa

? Kuhakikisha mipango ya kukuza uchumi wa taasisi ipo

? Kuhakikisha Mwajiri anatoa vifaa vya kazi kwa wakati

? Kuendeleza uhusiano bora mahali pa kazi

? Kuelimisha Wafanyakazi namna ya kuepuka migogoro kazini

? Kuhakikisha taratibu za kazi zinazingatiwa na wahusika wote

? Kuwa kiungo kati ya Wafanyakazi na Menejimenti


Masuala ya kiutendaji na TUICO ili kuondoa migongano kazini

? Masuala ya kiutendaji ni mambo mbalimbali yaliyoainishwa kwenye Sheria, Kanuni, Sera mbalimbali ambayo yamepitishwa na Mamlaka husika ili kufanikisha Malengo ya Taasisi.

? Masuala ya kiutendaji husimamiwa na Menejimenti ili kufanikisha utekelezaji wake, kwa mujibu wa maelekezo ya mamlala ya juu

? Wajibu wa TUICO ni kuhakikisha kuwa hakuna ukiukwaji wa haki na maslahi ya Wafanyakazi katika utekelezaji wa masuala ya kiutendaji.


Tofauti

? Menejimenti inatekeleza masuala ya utendaji ili

kufanikisha malengo na nidhamu kazini

? TUICO inahakikisha kuwa wakati wa utekelezaji hakuna athari kwa Wafanyakazi ili kupata tija

? Menejimenti inawajibika kutoa taarifa ya utekelezaji kwa mamlaka ya juu

? TUICO inawajibika kushauri namna nzuri ya utekelezaji wa suala husika na kuelimisha Wafanyakazi juu ya faida na athari zake

? Masuala ya kiutendaji ni ya Kikanuni zaidi, jukumu kubwa ni kwa Menejimenti kufanikisha

? TUICO husimamia na kuona kuwa masuala hayo hayaleti madhara kazini.


Namna ya kujenga na kuwasilisha hoja

? Hoja lazima iwe na misingi ya Sheria, Kanuni, Sera au Mikataba

? Hoja lazima iwe na Mmiliki
? Hoja lazima iwe na nguvu ya ushawishi (nguvu ya hoja na siyo Hoja ya Nguvu)

? Hoja iwe imefanyiwa uta?ti wa kina kabla ya kuwasilishwa

? Hoja ibebe malengo ya Taasisi na maslahi ya wengi

? Muwasilishaji wa hoja asiwe na mtizamo hasi juu ya upande mwingine wakati wa uwasilishaji

? Hoja ziandaliwe mapema na kuwasilishwa kwa wakati unaofaa
Read More of this Article in TUICO Newsletter

Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Kamati ya Wanawake TUICO wakiwa na Viongozi wa Hospitali ya Meta, Mbeya, kwenye siku ya Wanawake Duniani 07/03/2018

............................................................................................................

Other articles

DHANA YA AFYA NA USALAMA KAZINI

Usalama na Afya Kazini (OHS) ni azma mahususi inayolenga kulinda Usalama, Afya na Ustawi wa watu wote walio katika ajira iliyo rasmi.

published on 2018-08-21 06:24:22
By Silpha Kapinga

CALL FOR PROPOSALS

Call for proposals to supply TUICO with an accounting software. Deadline COB 30th May 2019 [VIEW FILE]

published on 2019-05-15 04:56:46
By Sebastian Okiki

PROHIBITING VIOLENCE AND HARASSMENT IN THE WORLD OF WORK

More than 800 million women have experienced some form of violence and harassment, ranging from physical assault to verbal abuse, bullying and intimidation...

published on 2019-06-10 04:27:32
By TUICO and IUF