Waziri Mwinyi alipongeza JKT kwa...
Waziri Mwinyi alipongeza JKT kwa mwanzo mzuri ujenzi ukuta wa Mererani
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt . Hussein Mwinyi (Mb) mwishoni mwa Juma alifanya ziara Mererani Wilayani Simanjirona kujionea ujenzi wa ukuta kuzunguuka yalipo machimbo ya madini ya Tanzanite kazi ambayo inafanywa na Jeshi la Kujenga Taifa.
Waziri Mwinyi akiwa ziarani hapo alipata wasaa wa kuzunguuka eneo lote la Kilometa 24.5 unapopita Mkuza na kujionea kazi inayoendelea kufanywa kwa ufanisi wa hali ya juu na Jeshi la Kujenga Taifa.
Akizungumza mara baada ya kukagua eneo la mradi Waziri Mwinyi alilipongeza JKT kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa mda mfupi kinyume na ambavyo yeye alikuwa akitarajia.
“Nimefarijika sana na kazi mliyoifanya, mmenipa faraja na matumaini makubwa kuwa kazi hii itaenda sambamba na ratiba yenu ya miezi sita mliyoiweka lakini mimi binafsi naomba muimalize mapema zaidiâ€.Alisisitiza Dkt. Mwinyi
Dkt Mwinyi aliutaka uongozi wa JKT kuifanya kazi hii kwa ufasi mkubwa na wahali ya juu kwani Jeshi litapimwa kwa jukumu hili na nyuma yake kuna macho ya watu yanaangalia.
Akasisitiza kuwa hata Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ana imani na Jeshi ndiyo maana jukumu hili akalileta kwetu ili likamilike kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa, hivyo hakikisheni kazi hii inafanyika kwa kiwango na wakati kama ilivyopangwa.
Aidha Waziri Mwinyi alipongeza Uongozi wa Wilaya ya Simanjiro kwa ushirikiano mkubwa ulioneshwa na wakazi wa M...
Habari Mpya
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ul...
April 12, 2018 -
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli Ameliagiz...
April 07, 2018 -
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Martin Busungu amemthibitishia...
April 07, 2018 -
Lilikuwa ni tukio la kusismua pale Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania M...
April 07, 2018