Rais Magufuli awapandisha vyeo Ma...

Rais Magufuli awapandisha vyeo Maafisa JWTZ
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mhe. Dkt . John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi kwa ngazi mbalimbali leo Aprili 12, 2018.
Akitangaza kupandishwa vyeo kwa maafisa hao Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo aliwataja waliopanda vyeo kuwa ni Meja Jenerali PP Masao anakuwa Luteni Jenerali huyu ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa Monduli na pia amempandisha Brigedia Jenerali HS Kamunde kuwa Meja Jenerali.
Mhe. Rais pia amewapandisha Makanali 28 kuwa Mabrigedia Jeneralia wakuu hao ni kama ifuatavyo:- Kanali DD Malugu ambaye ni Daktari , Kanali JJ Mwaseba ni mwambata Jeshi nchini Uingereza, Kanali AS Mwami niMwambata Jeshi nchini India, Kanali RK Kapinga, Kanali CD Katenga, Kanali ZS Kiwenge, Kanali MA Mgambo, Kanali AMAlfonce Mwambata Jeshi nchini Zimbabwe na Kanali AP Mutta Mwambata Jeshi nchini Marekani.
Wengine ni Kanali AB Chakila alikuwa nchini Kongo DRC, Kanali MG Mhagama, Kanali VM Kisiwi, Kanali CE Msolla, Kanali SM Mzee, Kanali CJ Ndyege, Kanali AM Mhona, Kanali RC Ng’umbi Mwambata Jeshi nchini China, Kanali SJ Mkande, Kanali AC Sibuti, Navy Capt MM Mmanga, Kanali IS Ismail na Kanali MA Mkeremi Mpambe wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wengine ni Kanali GS Mhize, Kanali MA Machanga, Kanali Gwaya, PS Simule na Kanali ME Gaguti ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambapo naye Mkuu wa Majeshi amemuomba Mhe. Rais amtumie kwa ajili ya kup...
Latest News
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ul...
April 12, 2018 -
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli Ameliagiz...
April 07, 2018 -
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Martin Busungu amemthibitishia...
April 07, 2018 -
Lilikuwa ni tukio la kusismua pale Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania M...
April 07, 2018