Katibu Mkuu Ulinzi atembelea Ujen...
Katibu Mkuu Ulinzi atembelea Ujenzi wa Ukuta Mererani
Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT, Dkt. Florens Turuka amefanya ziara ya kutembelea Mradi wa ujenzi wa ukuta kuzunguka eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite - Mererani unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Katibu Mkuu amefanya ziara hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza huku ikiwa na lengo la kutembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ukuta kuzunguka eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite – Mererani yaliyopo Wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara.
Utekelezajia wa mradi huu ni agizo la Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu alilolitoa tarehe 20 Septemba, 2017 kwa Mkuu wa Majeshi kwa kulitaka Jeshi la Kujenga Taifa kujenga uzio kuzunguka eneo lote la machimbo kwa lengo la kuzuia utoroshaji holela wa madini aina ya Tanzanite pasipo kulipiwa kodi.
Akitoa Taarifa kwa Katibu Mkuu, kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Mkuu wa Operesheni ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Ruvu JKT, Kanali Charles Mbuge alisema mradi umeanza rasmi tarehe 01 Novemba, 2017 baada ya maandaizi kukamilika ikiwa ni pamoja na kutumwa kwa fedha za kugharamia ujenziwa ukuta wenye mzingo wa kilomita 24.5 uliotarajiwa kukamilishwa ndani ya miezi sita ifikapo tarehe 30 Aprili, 2018.
Hadi sasa ambapo ni takribani ya kipindi cha miezi miwili tangu kuanza utekelezaji wa mradi huo, umeshakamilika kwa asilimia 80. kulingana na malengo waliyojiwekea wanatarajia kukamilisha mradi huo ifikapo tarehe 31 Januari, 2018 alisema Kanali Mbuge.
Siri ya mafanikio yal...
Habari Mpya
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ul...
April 12, 2018 -
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli Ameliagiz...
April 07, 2018 -
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Martin Busungu amemthibitishia...
April 07, 2018 -
Lilikuwa ni tukio la kusismua pale Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania M...
April 07, 2018