Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na J...
Katibu Mkuu wa Wizara ya ulinzi na JKT, Dr. Frolens Turuka alitembelea Kamandi ya Wanamaji (Navy) jijini Dar se salaam hivi karibuni Kwa ajili ya kujionea Utendaji na Utekelezaji wa Majukumu na Kufahamu changamoto zinazoikabili kamandi hiyo.
Katika hotuba iliyosomwa na Mkuu wa Kamandi, Meja Jenerali Richard Makanzo ilielezea historia fupi ya kuanzishwa kwa Kamandi hiyo tangu 6 Dec 1971, Kamandi hiyo ikiwa na jumla ya Vikosi pamoja na Viteule vilivyoko katika mikoa inayozungukwa na bahari na maziwa makubwa. Pamoja na hayo ameeleza majukumu ya asili ya kamandi hiyo kuwa ni Ulinzi wa Mipaka ukanda wa bahari na maziwa makubwa..
Katibu Mkuu huyo amepata nafasi ya kujionea maeneo mbalimbali ndani ya kamandi hiyo ikiwemo Maegesho ya Meli vita, Karakana ya kutengenezea Meli na baadhi ya Vipuli vya meli, Pia ameona ukarabati wa Meli ya utawala (Kasa) unaoendelea kupitia kampuni ya SONGORO.
Aidha, Katibu Mkuu Dr. Frolence Turuka, amepongeza shughuli zote zinazofanywa na kamandi hiyo, amesema kuwa anao muda wa kujifunza mengi kutoka katika Kamandi ya Wanamaji.
Zaidi ya hayo, amesema kuwa Kamandi hiyo inayo fursa kubwa ya kutekeleza sera ya Mh. Rais John Pombe Magufuli “Tanzania ya Viwanda†kwa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza boti ndogo ndogo na spea zake kwa ajili ya wavuvi wadogo wadogo ili kuchangia pato la Taifa.
Lakini pia, ameshauri Kamandi hiyo kuangalia fursa zaidi ya kufanya mambo makubwa kwa kuwa tayari imejenga mahusiano makubwa na kampuni za kutengeneza meli, kwa kuangalia maeneo makubwa...
Habari Mpya
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ul...
April 12, 2018 -
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli Ameliagiz...
April 07, 2018 -
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Martin Busungu amemthibitishia...
April 07, 2018 -
Lilikuwa ni tukio la kusismua pale Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania M...
April 07, 2018