TUICO
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO)

Kuhusu Sisi

Kuhusu Sisi

Sisi ni nani

Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) ni chama huru cha wafanyakazi kilichoanzishwa mwaka 1995. Tunahamasisha wafanyakazi kujiunga na Chama na kuwawakilisha katika sekta nne nchini Tanzania: viwanda, biashara, taasisi za fedha, na huduma na ushauri. TUICO ina wanachama zaidi ya 150,000.

Namna wanachama wanavyowakilishwa

Tawi mahali pa kazi huwawezesha wanachama kuwasilisha hoja zao, kushiriki katika maamuzi ya Chama na kuhamasishana pamoja na wafanyakazi wenzao. Ngazi za mikoa na Kanda huunganisha matawi na Chama. Katika ngazi ya Taifa, Kamati ya Utendaji ya Taifa, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu hutekeleza majukumu kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

Tunawakilisha wanachama katika masuala ya mahali pa kazi, tunajadiliana na kufuatilia utekelezaji wa Mikataba ya Hali Bora, na tunatoa elimu kwa wafanyakazi. Tunashirikiana na waajiri, serikali na vyama vingine vya wafanyakazi katika masuala ya sera za kazi na mazingira ya kazi.

TUICO kwa Ufupi

1995

Kuanzishwa

150K+

Wanachama

4

Sekta

8

Kanda

22

Ofisi za Mikoa

3

Ofisi Ndogo

Mwelekeo wa Chama

Dira na Dhima

Dira

Kuwa Chama imara na cha kidemokrasia kinachotoa huduma bora kwa wanachama wake.

Dhima

Kutoa huduma bora, zenye viwango vya juu, na zinazokidhi mahitaji ya wanachama.

Tunachofanya

Maeneo ya Kimkakati

Maeneo muhimu yanayoongoza utekelezaji wa vipaumbele vya TUICO.

Soma Mpango Mkakati →

Utawala wa Chama

Vikao vya Kikatiba

Vikao hivi hufanyika ili kusimamia shughuli za Chama katika ngazi mbalimbali kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.

Tawi

Halmashauri ya Tawi

Mara mbili kwa mwaka, Juni na Desemba

Mkutano wa Wanachama wote wa Tawi

Mara moja kwa mwaka, Septemba

Mikutano ya Wafanyakazi wote

Mara moja kwa mwaka, Desemba

Kamati ya Wanawake ngazi ya Tawi

Mara moja kwa mwaka, Juni

Mkoa

Kamati ya Utendaji ya Mkoa

Mara mbili kwa mwaka, Februari na Agosti

Kamati ya Wanawake ngazi ya Mkoa

Mara moja kwa mwaka, Julai

Kanda

Kamati ya Utendaji ya Kanda

Mara moja kwa mwaka, Oktoba

Mkutano Mkuu wa Kanda

Mara moja katika kipindi cha miaka mitano

Taifa

Kamati ya Utendaji ya Taifa

Mara mbili kwa mwaka, Aprili na Desemba

Baraza Kuu

Mara moja kwa mwaka, Aprili

Kamati ya Wanawake ngazi ya Taifa

Mara moja kwa mwaka, Agosti

Kamati ya Vijana ngazi ya Taifa

Mara moja kwa mwaka, Agosti

Mkutano Mkuu wa Taifa

Mara moja katika kipindi cha miaka mitano

Kamati ya Wafanyakazi wenye Ulemavu ngazi ya Taifa

Mara moja kwa mwaka, Agosti