Sekta
Biashara
Kuhusu Sekta
Sekta ya Biashara inahusisha wafanyakazi wanaofanya kazi katika biashara, shughuli za uuzaji wa jumla na rejareja, usambazaji, pamoja na taasisi zinazohusiana na biashara nchini Tanzania. TUICO inawakilisha wafanyakazi katika sekta hii katika masuala yanayohusu mazingira ya ajira, mishahara, haki za wafanyakazi, majadiliano ya pamoja, na hifadhi ya jamii. Sekta hii inajumuisha maeneo mbalimbali ya biashara ambapo utekelezaji wa haki za ajira, uwakilishi madhubuti wa wafanyakazi, na mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi na waajiri huchangia mazingira imara na endelevu ya biashara.
Mifano ya maeneo ya kazi
- Biashara na maduka ya rejareja
- Nishati na miundombinu ya huduma
- Utafiti na uchimbaji wa mafuta, gesi na madini
- Usafirishaji wa mizigo na bandari kavu
- Mialo na masoko ya samaki
Hii ni mifano. Kwa orodha kamili, soma kanuni ya 13.2 ya Kanuni za Katiba ya TUICO za mwaka 2021. Hujui eneo lako la kazi linaangukia sekta gani? Tuambie mahali unapofanya kazi kupitia fomu ya maelezo ya uanachama.
Mkuu wa Sekta
Adv. Prosper Mrema
Mkuu wa Sekta ya Biashara
Sekta Nyingine
Gundua Sekta Nyingine za TUICO
Viwanda
Sekta ya Viwanda inahusisha wafanyakazi wanaofanya kazi katika uzalishaji, usindikaji, mitambo ya uzalishaji, uhandisi,...
Angalia Sekta →Taasisi za Fedha
Sekta ya Taasisi za Fedha inahusisha wafanyakazi wanaofanya kazi katika benki, kampuni za bima, taasisi za fedha ndogo,...
Angalia Sekta →Huduma na Ushauri
Sekta ya Huduma na Ushauri inahusisha wafanyakazi wanaofanya kazi katika sekta za huduma, kampuni za ushauri, huduma za...
Angalia Sekta →