KUHUSU TUICO

HISTORIA YA TUICO

Harakati za vyama vya wafanyakazi Tanzania zimepitia katika vipindi tofauti vya kisiasa na kiuchumi. Harakati hizo ziliendeshwa wakati wa ukoloni na baada ya uhuru. Kabla ya uhuru (Wakati wa Ukoloni) Vyama vya Wafanyakazi viliendeshwa kwa uhuru na usawa lakini baada ya uhuru chama tawala kilidhibiti uhuru na usawa wa Vyama vya Wafanyakazi. Kwa mfano, kati ya mwaka 1964 na 1978 NUTA ilikuwa ni mshirika wa Tanganyika African National Union (TANU).Pia kati ya miaka ya 1979 hadi 1991 iliyokuwa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania (JUWATA) ilikuwa ni moja ya Jumuiya muhimu ya chama tawala (CCM). Tofauti hizi hazikuathiri tu miundo ya Vyama vya Wafanyakazi lakini pia zilichangia kubadili tabia na mitizamo ya Vyama vya Wafanyakazi hapa Tanzania

Trade Union have always been forced by circumstantial events to shape themselves to suit the socio-economic developments prevailing at that time. The wind of change that shook the country in the 1990’s also effected the trade union movement. In year 2000 eleven (11) free Trade Unions were formed, and they are all affiliated to the national center that is Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA). Tanzania Union of Industrial and Commercial Workers (TUICO being one of them.) TUICO as a new democratic workers union is currently operating in new environment dominated by the free market economy. The union organizes members form Industries, Commercial, Finance, Institutions, Services and Consultancy.

Vyama vya wafanyakazi vimekuwa vikisukumwa na matukio mbalimbali yanayotokana na mabadiliko katika mifumo ya kijamii na kiuchumi, aidha mabadiliko ya kiuchumi yaliyoikumba nchi miaka ya 90 pia yalibadili mfumo wa vyama vya wafanyakazi.

Mwaka 2000 Vyama huru 11vya Wafanyakazi hapa Tanzania viliundwa kupitia Sheria ya Vyama vya Wafanyakazi Na. 10 ya mwaka 1998 na vyote vilishirikishwa katika Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA). Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) ni miongoni mwa Vyama hivyo.

TUICO ni Chama cha Wafanyakazi cha kidemokrasia kinachofanya kazi katika mazingira mapya ya uchumi wa soko huria (free market economy). TUICO inahamasisha wafanyakazi kutoka Sekta za Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri kuwa wanachama. Kwa Tanzania, muda wa uongozi katika vyama vya wafanyakazi ni miaka mitano (5). Uchaguzi mkuu wa nne wa kitaifa wa TUICO ulifanyika mwaka 2015 na viongozi waliopo madarakani hivi sasa kutoka ngazi ya tawi hadi ngazi ya Taifa walichaguliwa .

Muundo wa TUICO

TUICO imeundwa na Sekta kuu nne (4) ambazo ni; Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri. Pia kuna Idara nne (4) ambazo ni; Fedha; Utumishi na Utawala, Elimu na Uhamasishaji; Wanawake, Afya na Usalama. Vilevile kuna Vitengo vinne (4) ambavyo ni; Ukaguzi wa Ndani, Sheria, Uhamasishaji na Vijana pamoja na Utafiti na Takwimu:

  1. Makao Makuu
  2. Ofisi 22 za Mikoa
  3. Ofisi 8 za Kanda
  4. Ofisi 865 za halmashauri za Matawi

VIKAO VYA CHAMA KIKATIBA

Muundo wa Chama unaanzia kwenye ngazi ya Tawi (sehemu ya kazi) ambapo ndipo kwenye wanachama, wakifuatiwa na ngazi ya Mkoa, ngazi ya Kanda na ngazi ya Taifa. Vikao vya Chama ni kama ifuatavyo:-

Na Ngazi Vikao Muda wa vikao
1 Tawi
  1. Kikao cha Halmashauri ya Tawi
  2. Kikao cha wanachama
  3. Mkutano wa wafanyakazi wote
  • Kila baada ya miezi mitatu
  • Mara moja kila baada ya miezi 6
  • Mara moja kwa mwaka
2 Mkoa
  1. Kamati ya Utendaji ya Mkoa
  2. Mkutano Mkuu wa Mkoa
  • Mara moja kila baada ya miezi sita
  • Mara moja kila baada ya miaka mitano
3 Kanda
  1. Kamati ya Utendaji ya Kanda
  2. Mkutano Mkuu wa Kanda
  • Mara moja kwa mwaka
  • Mara moja kwa mwaka
4 Taifa
  1. Kamati ya Utendaji Taifa
  2. Baraza Kuu
  3. Mkutano Mkuu
  • Mara moja kila baada ya miezi sita
  • Mara moja kwa mwaka
  • Mara moja kila baada ya miaka mitano

Mahisiano ya chama; Kitaifa na Kimataifa

Katika kujenga ushirikiano na mshikamano miongoni mwa Vyama vya Wafanyakazi, TUICO imejishirikisha na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA). Aidha chama kimejishirikisha na Mashirikisho ya Vyama vya Wafanyakazi vya Kimataifa kama UNI, PSI, IndustriALL, BWI, IUF pamoja na Streetnet International.

Mipango ya TUICO

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, TUICO imepiga hatua nzuri katika Nyanja za uhamasishaji, elimu, mikataba ya hali bora na utetezi. TUICO imepanga kuimarisha na kukuza shughuli za chama pamoja na kutoa huduma bora kwa wanachama wake. Mfumo mpya wa Mawasiliano wa TUICO umeimarisha utendaji wa chama na kuwezesha Chama kutoa huduma bora zaidi kwa wanachama wake.