SEKTA YA VIWANDA

UTANGULIZI

Sekta hii ilianzishwa mwaka 1995 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wafanyakazi na wanachama wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vya uzalishaji na uchakataji. Huduma hizo ni pamoja na; Mikataba mizuri ya ajira na utatuzi wa migogoro.

Kazi za Sekta

1. Kupendekeza maboresho ya Sheria za Kazi

2. Kuhamasisha na kuingiza wanachama wapya

3 Kuelimisha wafanyakazi kuhusu haki na maslahi yao kazini.

4 Kujenga na kudumisha mahusiano bora mahala pa kazi.

5 Kusimamia utekelezaji wa Mikataba, Maazimio na Matamko ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) yaliyoridhiwa na Nchi yetu

6 Kushiriki katika Mabaraza ya Wafanyakazi

7 Kushiriki katika mikutano mbalimbali ya wadau

8. Kuwakilisha wanachama katika utatuzi wa migogoro ya kikazi katika ngazi zote

9. Kujadili na kufunga mikataba ya hali bora (CBA) baina ya Chama na Waajiri

TPCC Workers
Wafanyakazi wa kiwanda cha saruji cha TPCC wakiwa wamezingatia matumizi sahihi ya vifaa vya kinga wakiwa kazini