KITENGO CHA TAKWIMU NA UCHUMI

    Utangulizi

    Kitengo hiki ni moja kati ya vitengo vinne vya Chama. Kitengo kinahusika na masuala ya Takwimu pamoja na Utafiti katika Chama. Hii husaidia Chama wakati wa upangaji mipango yake ya kila Mwaka.

    Kazi za Kitengo

    1. Kukusanya na kuchambua taarifa mbalimbali kutoka Makao Makuu na Ofisi za Mikoa.

    2. Ufuatiliaji na ukusanyaji wa kodi kutoka majengo yote yanayomilikiwa na Chama.

    3. Kufuatilia na kusimamia kodi ya ardhi, majengo na ukarabati wa ofisi za Chama

    4. Kufanya tafiti kuhusu masuala ya kiuchumi na kijamii kutoka katika vyanzo mbalimbali kwa matumizi ya Chama.

    5. Kitengo pia hutumika kama maktaba endapo itahitajika kufanya marejeo kuhusu taarifa na machapisho mbalimbali ndani ya Chama.