FEDHA NA UTAWALA

  Utangulizi

  Idara ya Utumishi na Utawala ni moja ya Idara za TUICO inayohusika na watumishi wa TUICO na Utawala. Idara hii inahudumia wafanyakazi wote wa Chama katika masuala ya Rasilimali watu na Utawala

  Kazi za Idara

  Kazi zinazosimamiwa na Idara hii ni kama ifuatavyo;

  1. Kubuni na kupanga mahitaji ya Rasilimali watu

  2. Kusimamia nidhamu za Watumishi wote

  3. Kutoa ushauri katika mashauri ya kinidhamu

  4. Kufanya tathmini ya ufanisi wa Watumishi

  5. Kushughulikia mambo ya kikazi ya Watumishi

  6. Kupandisha vyeo, mishahara, likizo na fidia kwa Watumishi

  7. Kuthibitisha kazini Watumishi

  8. Kutoa Elimu na mafunzo kwa Watumishi

  9. Kutoa huduma ya usafiri, kushughulika na huduma za kila siku za kiofisi.

  10. Kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kazi kulingana na wakati

  11. Kuandaa na kurekebisha mpango wa huduma wa Chama

  12. Kushughulikia motisha kwa watumishi kwa dhumuni la kuleta ufanisi katika kazi

  13. Kusimamia na kuratibu mikutano ya Chama.


  Kwa ujumla Idara hii inahusika na kazi za kiutawala na mambo mengine binafsi ya Watumishi kwa kushirikiana kwa karibu na ofisi ya Katibu Mkuu.