SEKTA YA BIASHARA

UTANGULIZI

Sekta hii ilianzishwa mwaka 1995 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wafanyakazi na wanachama katika taasisi za kibiashara mfano ;Nishati, Mafuta na Gesi, maduka makubwa (super markets) na kampuni za uuzaji magari.

Kazi za Sekta

1. Kushiriki katika Mabaraza ya Wafanyakazi

2. Kuhamasisha na kuingiza Wanachama wapya

3. Kushiriki katika mikutano mbalimbali ya wadau

4. Kuwakilisha wanachama katika utatuzi wa migogoro ya kikazi katika ngazi zote

5. Kutoa Elimu kwa Wanachama, Viongozi na Wafanyakazi juu ya Sheria za kazi na Mbinu za Majadiliano

6. Kujadili na kufunga Mikataba ya Hali Bora (CBA) baina ya Chama na Waajiri

7. Kushirikiana na Mashirikisho ya Vyama vya Wafanyakazi Duniani ( Global Union Federations)

8. Kusimamia utekelezaji wa Mikataba, Maazimio na Matamko ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) yaliyoridhiwa na nchi yetu.