NAMNA YA KUJIUNGA NA TUICO

TUICO ni nini?

Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) ni Chama huru cha Wafanyakazi kinachosimamia Wafanyakazi kutoka Sekta za Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri
Chama kilianza kufanya kazi kama Chama huru cha Wafanyakazi Mwezi Januari Mwaka 1996 na kimejishirikisha na TUCTA(Link) na Mashirikisho ya Vyama vya Wafanyakazi vya Kimataifa. Kazi kubwa ya TUICO ni kulinda na kutetea haki na maslahi ya Wafanyakazi.

Faida ya Kuwa Mwanachama wa TUICO

Faida za kuwa Mwanachama wa TUICO ni pamoja na:-

1. Mwanachama kuwakilishwa na TUICO kwenye mgogoro unaomuhusu mwajiri na mfanyakazi

2. Mwanachama kuelimishwa kuhusu haki na wajibu wa Mwanachama

3. Kujadiliana na Mwajiri kwa lengo la kufunga Mkataba wa Hali

4. Bora ambao utaboresha ustawi wa Wanachama.

5. Kuwa na mshikamano na kufanya kazi pamoja na Wanachamawengine kutoka Sekta mbalimbali (ndani na nje ya nchi)

6. Kulinda na kutunza Ajira ya Mwanachama.

7. Haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi.

Watendaji wa TUICO hutembelea maeneo ya kazi kwa lengo la kuhamasisha wafanyakazi wajiunge na Chama. Ili kuwa Mwanachama unatakiwa ujaze fomu ya kisheria (TUF-15) (nakala tatu (3)) which are submitted to the Employer and the Union. ambazo zinawasilishwa kwa mwajiri na chama. Unaweza pia kutembelea ofisi ya chama ya mkoa na kujaza fomu hiyo ili baadae iwasilishwe kwa mwajiri wako.