IDARA YA FEDHA

    Utangulizi

    Hii ni moja ya Idara za Chama inayo shughulikia masuala yote ya fedha

    Kazi za Idara

    1. Kusimamia na kuhakikisha kuwa ada za Chama kutoka kwa wanachama zimekusanywa kwa wakati na zimehifadhiwa katika akaunti ya Chama

    2. Kutunza na kuhakiki taarifa zote zinazohusu mapato na matumizi ya Chama kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Chama.

    3. Kuhakikisha kuwa Chama kinatumia mapato kulingana na bajeti iliyopitishwa na Baraza Kuu.

    4. Kuripoti kwa Katibu Mkuu kuhusu mapato na matumizi yote yanayofanyika ndani ya chama.

    5. Kusimamia na kuelekeza matumizi sahihi ya mali za Chama kama vile magari, majengo na mashine na vifaa vya ofisi.