USHIRIKISHAJI

Ushirikishaji

TUICO imejishirikisha na Mashirikisho ya Vyama vya Wafanyakazi Duniani. Ifuatayo ni orodha ya Mashirikisho hayo;

Shirikisho hili linawakilisha Wafanyakazi zaidi ya milioni 50 katika nchi 140 kwenye sekta za madini/migodi, nishati na viwanda na inaimarisha mshikamano katika kupigania haki na mazingira mazuri ya kufanyia kazi duniani kote.SOMA ZAIDI Soma zaidi kuhusu Industriall >>>

Shirikisho hili limechangia miradi kadhaa ambayo ililenga kujenga uwezo zaidi wa Chama. Mfano hai ni mradi wa TEHEMA ambao ulifadhiliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Canada
(UNIFOR). Mradi huu ulikamilika Juni 30, 2018 na umeisaidia TUICO kuanzisha na mfumo rasmi wa mawasiliano ndani ya chama, kukarabati chumba maalum kwa ajili ya kuendeshea mafunzo ya TEHAMA, Manunuzi ya kompyuta mpakato 80 ambazo ziligawanywa kwa Wakuu wa Sekta, Idara, Vitengo, Makatibu wa Mikoa na chumba cha kufundishia TEHAMA.

Hili ni Shirikisho la Kimataifa linalowakilisha Wafanyakazi zaidi ya milioni Ishirini (20,000,000) katika nchi 163 Duniani. Shirikisho linapigania Haki za Binadamu, Haki za Kijamii na kusaidia kukuza na kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wafanyakazi walio katika Sekta ya Umma.
Soma zaidi kuhusu PSI >>>

TUICO na vyama vingine vitatu vyenye wanachama kutoka katika Taasisi za umma hapa Tanzania vimejishirikisha na PSI kwa lengo la kuboresha huduma kwa wanachama. PSI wamekuwa wakidhamini miradi ya kujenga uwezo kwa watumishi wa Umma juu ya Nishati, Upatikanaji wa huduma bora za Maji safi na salama, Ubinafsishaji wa huduma za Kijamii kwa Umma, mijadala ya kijamii pamoja na uelewa kuhusu haki kutokana na kodi.

Hili ni Shirikisho kubwa la Vyama vya Wafanyakazi Nchini Uholanzi linalowawakilisha zaidi ya Wanachama milioni moja na laki moja (1,100,000).
Soma zaidi kuhusu FNV >>>

TUICO ina ushirikiano mzuri na FNV ambao umelenga katika kujenga na kuimarisha uwezo wa Chama. FNV imesaidia Chama kuendesha mafunzo kwa watendaji na baadhi ya Wanachama katika maeneo ya Ufungaji wa Mikataba ya Hali Bora, Afya na Usalama na matumizi ya TEHAMA.

TNi muungaano unaowakilisha Vyama vyote vya wafanyakazi Afrika. Muungano huu una vyama shiriki 73 kutoka nchi 54 za Afrika na wanachama zaidi ya milioni Ishirini na tano (25,000,000)
Soma zaidi kuhusu OATUU >>>

OATUU inadhamini mradi wa PANAF. Kupitia mradi huu, TUICO imeweza kuanzisha na kuendesha Elimu kwa njia ya vikundi katika mikoa mbalimbali hapa Nchini.

Hili ni Shirikisho linaliwahusisha Wafanyakazi walio katika viwanda vya Saruji na Mbao. Shirikisho hili lilitokana na mkutano mkuu uliofanyika 9 Disemba 2005, ulioshirikisha Mashirikisho mawili ya Kimataifa yaani IFBWW na WFBW ambayo yaliungana na kuunda shirikisho jipya la wafanyakazi linalojulikana kama BWI (Building and Wood Workers’ International).
Soma zaidi kuhusu BWI >>>

TUICO imejishirikisha na BWI kwa kuwa baadhi ya wanachama wake wanatoka katika Sekta za viwanda vya Saruji na Mbao. Shirikisho hili limewezesha TUICO kuendesha mafunzo yenye kujenga uwezo wa viongozi, wanachama na wafanyakazi katika viwanda vinavyozalisha Saruji kwenye Sheria za kazi, Mikataba ya Hali Bora, nidhamu na uongozi bora katika chama.

Huu ni Shirikisho linalowaunganisha wafanyabiashara ndogondogo wa mitaani. Shirikisho hili lilianzishwa rasmi nchini Afrika ya Kusini katika mji wa Durban Mwezi Novemba Mwaka 2002. Lengo kuu la Shirikisho hili ni kukuza na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala nyeti yanayowahusu wafanyabiashara wa mitaani, masokoni na wamachinga.
Soma zaidi kuhusu Streetnet >>>

Hili ni shirikisho ambalo limedhamini miradi ya TUICO yenye lengo la kuwezesha chama kuhamasisha na kuingiza wanachama kutoka uchumi usio rasmi (informal economy).

Miradi hii inalenga kusaidia Chama katika kuhamasisha na kuingiza Wanachama Wapya kutoka katika Uchumi usio rasmi (Informal Economy). Mikutano na shughuli za uhamasishaji zimefanyika katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na soko la Buguruni, Karume, TAZARA, Temeke Sterio, Tabata, Machinga Complex, Mburahati, Ferry na Mabibo. Chama kimefanikiwa kupata Wanachama wapya kwenye maeneo hayo. Aidha Elimu imetolewa kwa Wakurugenzi na Madiwani kutoka Kanda ya Dar es salaam kuhusu umuhimu wa Vyama vya Wafanyakazi, Mikataba ya Hali Bora, Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Bima ya Afya na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Solidarity Centre has sponsored projects aimed at enhancing TUICO capacity to engage in publicity and recruitment of new members from informal economy. Out of this project, TUICO recruited ……new members from food selling market at Buguruni, fish market at Ferry area, hawkers centres at Karume, TAZARA, Machinga Complex, Mburahati and Mabibo areas. Solidarity Centre also facilitated seminars to directors and councilors from Dar es Salaam on the role of trade Union, collective bargaining agreement, social security funds, insurance funds and workers’ compensation fund.

Hili ni Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi la Kimataifa linalosimamia Ujuzi na Huduma kwa wafanyakazi. Shirikisho hili ni sauti ya Wafanyakazi zaidi ya milioni 20 kutoka Sekta ya huduma kote Duniani kupitia Vyama shiriki 900 katika Nchi 140. UNI inawakilisha wafanyakazi kutoka Sekta za Usafi na Usalama, Biashara, Fedha, Urembo na Nywele, TEHAMA, Vyombo vya Habari, Burudani, Sanaa pamoja na Huduma za Posta na usafirishaji, bima za jamii, michezo na utalii.
Soma zaidi kuhusu UNI >>>

Shirikisho hili limewezesha TUICO kuelimisha watendaji wa Chama kwenye Mbinu za Majadiliano ya Pamoja na Uhamasishaji. Kutokana na Elimu hii, Chama kimeweza kujenga timu nzuri ya Watendaji iliyowezesha Chama kufunga mikataba mingi ya Hali Bora na kuingiza Wanachama wapya

Ni Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Wafanyakazi linalowakilisha Wafanyakazi walioajiriwa katika Kilimo, Mashamba na Viwanda vinavyotengeneza Vyakula na Vinywaji, Mahoteli, Hifadhi, Migahawa na walio katika Viwanda vya Uchakataji Tumbaku. Shirikisho hili limewezesha TUICO kuwajengea uwezo Wafanyakazi Wanawake waliopo katika maeneo mbalimbali ya kazi.
Ssoma zaidi kuhusu IUF >>>

Ni Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Wafanyakazi linalowakilisha Wafanyakazi walioajiriwa katika Kilimo, Mashamba na Viwanda vinavyotengeneza Vyakula na Vinywaji, Mahoteli, Hifadhi, Migahawa na walio katika Viwanda vya Uchakataji Tumbaku. Shirikisho hili limewezesha TUICO kuwajengea uwezo Wafanyakazi Wanawake waliopo katika maeneo mbalimbali ya kazi .
Soma zaidi kuhusu Soliderity Center >>>

Kwa ushirikiano na Streetnet International, Shirikisho hili limedhamini miradi ya TUICO yenye lengo la kuwezesha chama kuhamasisha na kuingiza wanachama kutoka uchumi usio rasmi (informal economy).

Miradi hii inalenga kusaidia Chama katika kuhamasisha na kuingiza Wanachama Wapya kutoka katika Uchumi usio rasmi (Informal Economy). Mikutano na shughuli za uhamasishaji zimefanyika katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na soko la Buguruni, Karume, TAZARA, Temeke Sterio, Tabata, Machinga Complex, Mburahati, Ferry na Mabibo. Chama kimefanikiwa kupata Wanachama wapya kwenye maeneo hayo. Aidha Elimu imetolewa kwa Wakurugenzi na Madiwani kutoka Kanda ya Dar es salaam kuhusu umuhimu wa Vyama vya Wafanyakazi, Mikataba ya Hali Bora, Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Bima ya Afya na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Baraza la Vyama vya Wafanyakazi la Denmark (LO-FTF) lilianzishwa kwa ajili ya kujenga ushirikiano wa maendeleo kimataifa. Baraza hili lilianzishwa mwaka 1987 baada ya muungano wa mashirikisho mawili makubwa ya Wafanyakazi nchini Denmark; LO na FTF.
Soma zaidi kuhusu LO-FTF >>>

Baraza hili limesaidia chama katika masuala ya Afya na usalama kwa kuendesha mafunzo kwa watendaji wa TUICO katika mikoa yote pamoja na kuandaa Makala za Afya na Usalama kwa ajili ya kufundishia wanachama wetu katika mahala pa kazi. Aidha limewezesha chama kuunda Kamati za Afya na Usalama katika maeneo ya kazi