logo

Tanzania Union of Industrial and Commercial Workers
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri

logo

KUHUSU TUICO

HISTORIA YA TUICO

Harakati za vyama vya wafanyakazi Tanzania zimepitia katika vipindi tofauti vya kisiasa na kiuchumi. Harakati hizo ziliendeshwa wakati wa ukoloni na baada ya uhuru. Kabla ya uhuru (Wakati wa Ukoloni) Vyama vya Wafanyakazi viliendeshwa kwa uhuru na usawa lakini baada ya uhuru Vyama vya Wafanyakazi vilikuwa sehemu ya Chama Tawala. Kwa mfano, kati ya mwaka 1964 na 1978 NUTA ilikuwa ni sehemu ya Tanganyika African National Union (TANU).Pia kati ya miaka ya 1978 hadi 1991 Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania (JUWATA) ilikuwa ni moja ya Jumuiya muhimu ya Chama Tawala (CCM). Tofauti hizi hazikuathiri tu miundo ya Vyama vya Wafanyakazi lakini pia zilichangia kubadili tabia na mitizamo ya Vyama vya Wafanyakazi hapa Tanzania

TUICO ni Chama cha kipekee cha Wafanyakazi hapa Tanzania kinachohudumia Wafanyakazi kutoka Taasisi za Umma na Binafsi kinaundwa na Sekta Nne ambazo ni Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri. Vyama vya Wafanyakazi vimekuwa vikisukumwa na matukio mbalimbali yanayotokana na mabadiliko katika mifumo ya kijamii na kiuchumi, aidha mabadiliko ya kiuchumi yaliyoikumba nchi miaka ya 90 pia yalibadili mfumo wa Vyama vya Wafanyakazi.


Chama cha Wafanyakazi TUICO kilianzishwa mwaka 1995 pamoja na Vyama vingine 10 na kujishirikisha katika Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania Federation of Free Trade Union(TFTU) mwaka 1998 na baadae TUCTA (Trade Union Congress of Tanzania) mwaka 2001. .

MUUNDO WA TUICO

TUICO ina Sekta kuu nne (4) ambazo ni;

  • Viwanda
  • Biashara
  • Taasisi za Fedha
  • Huduma na Ushauri

TUICO ina Idara kuu nne (4);

  • Fedha na Utawala
  • Elimu na Vijana
  • Sheria
  • Wanawake, Afya na Usalama

TUICO ina Vitengo vitatu (3);

  • Uhamasishaji na Uhusiano wa Kimataifa
  • Ukaguzi wa Ndani
  • Uchumi, Takwimu na TEHAMA

TUICO ina Ofisi zifuatazo;

  • Makao Makuu
  • Ofisi 8 za Kanda
  • Ofisi 22 za Mikoa
  • Ofisi 4 Ndogo za Mikoa

VIKAO NA MIKUTANO YA CHAMA KIKATIBA

Muundo wa Chama unaanzia kwenye ngazi ya Tawi (sehemu ya kazi) ambapo ndipo kwenye wanachama, wakifuatiwa na ngazi ya Mkoa, ngazi ya Kanda na ngazi ya Taifa. Vikao vya Chama ni kama ifuatavyo:-

Na Ngazi Vikao na Mikutano Muda
1 Tawi
  1. Kikao cha Halmashauri ya Tawi
  2. Mkutano wa wanachama
  3. Mkutano wa wafanyakazi wote
  • Kila baada ya miezi mitatu
  • Mara moja kila baada ya miezi 6
  • Mara moja kwa mwaka
2 Mkoa
  1. Kamati ya Utendaji ya Mkoa
  2. Mkutano Mkuu wa Mkoa
  • Mara moja kila baada ya miezi sita
  • Mara moja kila baada ya miaka mitano
3 Kanda
  1. Kamati ya Utendaji ya Kanda
  2. Mkutano Mkuu wa Kanda
  • Mara moja kwa mwaka
  • Mara moja kila baada ya miaka mitano
4 Taifa
  1. Kamati ya Utendaji Taifa
  2. Baraza Kuu
  3. Mkutano Mkuu
  • Mara moja kila baada ya miezi sita
  • Mara moja kwa mwaka
  • Mara moja kila baada ya miaka mitano

MAHUSIANO YA CHAMA KITAIFA NA KIMATAIFA

Katika kujenga Ushirikiano na Mshikamano miongoni mwa Vyama vya Wafanyakazi, TUICO imejishirikisha na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA). Aidha Chama kimejishirikisha na Mashirikisho ya Vyama vya Wafanyakazi vya Kimataifa kama UNI, PSI, IndustriALL, BWI, IUF pamoja na Streetnet International.

MPANGO MKAKATI

TUICO ina Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (5) unaotekelezwa katika kipindi cha Mwaka mmoja mmoja katika maeneo kumi (10) muhimu ikiwa ni pamoja na Uhamasishaji, Utoaji wa Elimu na Ufungaji wa Mikataba mbalimbali.