logo

Tanzania Union of Industrial and Commercial Workers
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri

logo

FEDHA NA UTAWALA

    Utangulizi

    Idara ya Fedha na Utawala inahusika na masuala ya Fedha, Rasilimali Watu na Utawala kwa Watumishi wa TUICO.

    MAJUKUMU YA IDARA

    Idara hii ina Majukumu yafuatayo;

    1. Kuhakikisha mapato ya Chama yanakusanywa kwa wakati na kutunza kumbukumbu za Fedha.

    2. Kusimamia Mapato ya Chama yanayotokana na vyanzo mbalimbali.

    3. Kuwezesha na Kudhibiti matumizi ya Fedha za Chama

    4. Kununua na kusimamia matumizi ya Mali za Chama kama vile Majengo, Vyombo vya Usafiri na Vifaa vya Ofisi.

    5. Kubuni, Kupanga mahitaji na matumizi ya Rasilimali Watu.

    6. Kusimamia nidhamu za Watumishi wote.

    7. Kufanya tathmini ya ufanisi wa Watumishi.

    8. Kushughulikia masuala yote yanayohusu Watumishi.

    9. Kusimamia Utekelezaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya kazi kulingana na wakati.

    10. Kuandaa na kurekebisha Muundo wa Utumishi na Mpango wa Motisha kwa Watumishi.

    11. Kushughulikia masuala mengine ya Kiutawala yatakayojitokeza mahala pa kazi.