logo

Tanzania Union of Industrial and Commercial Workers
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri

logo

KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI

    UTANGULIZI

    kitengo hiki kinapitia Taarifa za Uhasibu, Fedha na Uendeshaji wa shughuli za Chama.

    MAJUKUMU YA KITENGO

    1. Kupitia na Kushauri Chama juu ya uimara wa Mfumo wa Udhibiti wa ndani hasa juu ya Mapato na Matumizi.

    2. Kufuatilia kama Chama kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.

    3. Kupitia na kutathmini malengo yaliyopangwa na kubaini vihatarishi vinavyoweza kuathiri shughuli za uendeshaji wa Chama.

    4. Kutoa taarifa na mapendekezo mbalimbali ya matokeo ya Ukaguzi ili kuongeza thamani na kuboresha Utendaji wa Chama.