logo

Tanzania Union of Industrial and Commercial Workers
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri

logo

Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Tumefurahishwa na maamuzi yako ya kujiunga na Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO). Tovuti hii inaeleza shughuli na matukio mbalimbali ya chama

TUICO ni Chama cha kipekee cha Wafanyakazi hapa Tanzania kinachohudumia Wafanyakazi kutoka Taasisi za Umma na Binafsi kinaundwa na Sekta Nne ambazo ni Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri. Vyama vya Wafanyakazi vimekuwa vikisukumwa na matukio mbalimbali yanayotokana na mabadiliko katika mifumo ya kijamii na kiuchumi, aidha mabadiliko ya kiuchumi yaliyoikumba nchi miaka ya 90 pia yalibadili mfumo wa Vyama vya Wafanyakazi.


Chama cha Wafanyakazi TUICO kilianzishwa mwaka 1995 pamoja na Vyama vingine 10 na kujishirikisha katika Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania Federation of Free Trade Union(TFTU) mwaka 1998 na baadae TUCTA (Trade Union Congress of Tanzania) mwaka 2001.


DIRA NA DHAMIRA

DIRA

Kuwa na Chama Imara cha Kidemokrasia kinachotoa Huduma Bora kwa Wanachama.

DHAMIRA

Kutoa Huduma Bora zenye Viwango vya juu zinazokidhi mahitaji ya Wanachama.